Taarifa ya Habari 22 Agosti 2024

City - Swahili.jpg

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Wazazi wapya hivi karibuni wataweza anza pokea malipo yao ya uzeeni juu ya malipo ya likizo ya wazazi yanayo wekezwa na serikali, sheria ziki tarajiwa kuwasilishwa ndani ya bunge la shirikisho hii leo Alhamis 22 Agosti.


Sheria hizo zitaweza waruhusu wazazi kupokewa asilimia 12 ya malipo ya uzeeni na, iwapo sheria hizo zitapitishwa zita anza kutumika kuanzia Julai 2025. Hatua hiyo itasaidia familia 180,000 zinazo tumia likizo inayo wekezwa na serikali baada yakuzaa mtoto. Waziri wa huduma za jamii Amanda Rishworth, ame eleza makala ya Radio National ya shirika la habari la ABC kwamba, sheria hizo zita boresha usawa wakijinsia.

 

Mageuzi kwa mfumo wa bima ya kitaifa ya ulemavu, yanatarajiwa kupitishwa ndani ya bunge la taifa. Serikali inajaribu kudhibiti gharama ya mfumo huo wenye thamani ya dola bilioni 46, ambayo bila mageuzi inatarajiwa kupita gharama ya Medicare ndani ya miaka mbili. Sheria hizo zita badilisha jinsi watu wenye ulemavu wanavyo tumia uwekezaji na huduma gani wanaweza pata zitabadilika. Makundi mengi ya wanaharakati wa ulemavu, yana wasiwasi kuhusu jinsi mpango huo waku dhibiti gharama, uta wa athiri watumiaji.

Mamlaka ya usafiri wa anga ya Somalia imetishia kusimamisha safari zote za ndege za shirika la ndege la Ethiopia kuelekea nchini humo, vyombo vya habari vya serikali vilisema Jumatano, kitendo cha hivi karibuni katika mzozo wa muda mrefu unaohusu jimbo la Somaliland lililojitenga.

Addis Ababa ilisaini mapema mwaka huu mkataba wa maelewano na Somaliland kukodisha kilomita 20 za pwani katika kipindi cha miaka 50, kuiruhusu Ethiopia isiyo na bahari kufika kwenye pwani. Kwa upande wake, Somaliland ambayo ilitangaza uhuru wake kwa kujitenga na Somalia mwaka 1991, imesema Ethiopia itakuwa nchi ya kwanza kuitambua rasmi Somaliland kama taifa, hatua ambayo haijathibitishwa na Addis Ababa. Ndege za Ethiopian Airlines zinasafiri hadi mji mkubwa wa Somaliland wa Hargeisa, na mji mkuu wa Somalia Mogadishu na miji minne ya majimbo ya Somalia. Mamlaka ya anga ya Somalia (SCAA) imesema Ethiopian Airlines inayomilikiwa na serikali, shirika kubwa la ndege barani Afrika, halijashughulikia malalamiko ya hapo awali kuhusu “masuala ya uhuru” na limeondoa taarifa za safari kuelekea Somalia, na kubakiza tu namba za viwanja vya ndege”.

Tawala za kijeshi za Burkina Faso, Mali na Niger zimeliandikia barua baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zikishutumu Ukraine kwa madai kwamba inaunga mkono makundi ya waasi ya Afrika Magharibi katika eneo la Sahel. Hayo ni kulingana na nakala ya barua yao iliyokuwa imechapishwa kwenye mitandao ya kijamii. Msemaji huyo alisema kuwa wanamgambo wa eneo la Kaskazini mwa Mali wamepokea taarifa “muhimu” za kufanya mashambulizi ya mwezi Julai. Katika barua yao, nchi hizo zinazoongozwa na jeshi zimeliomba baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa “kuvichukulia hatua” vitendo vya Ukrainen kuzuia “vitendo vya ugandamizaji”. Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine hakuweza kutoa majibu ya haraka lakini Ukraine imekuwa mara kwa mara ikituhumu tawala hizo za kijeshi kwa madai yasiyokuwa na msingi na ya uongo.

Share