Sekta ya elimu ya juu yasema wanafunzi wakimataifa wamekuwa 'lishe ya mzinga' katika mjadala wa uhamiaji

Group of college grads

College friends have serious conversation after the graduation ceremony. Credit: SDI Productions/Getty Images

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Idadi ya wanafunzi wakimataifa itawekewa vikomo mwaka ujao, serikali inapojaribu kupunguza uhamiaji wa ng’ambo.


Waziri wa Elimu Jason Clare amesema hatua hiyo ita leta usawa zaidi katika sekta ya elimu yakimataifa ila, vyuo vingi vime pinga mpango huo.

Kwa ujumla, idadi ya wanafunzi 270,000 wataweza anza kusomea nchini Australia katika mwaka wa 2025.

Kutakuwa nafasi 145,000 katika vyuo vikuu vinavyo fadhiliwa na umma, sawia na viwango vya 2023 wakati sekta ya elimu ya ufundi itapungua kwa asilimia 20 kwa viwango vya kabla, na vitasalia na nafasi 95,000.

The Group of Eight, ni kundi linalo jumuisha vyuo vya Australia vinavyo fanya utafiti wa kina, vimesema vinakadiria kutakuwa mkato wa 30% katika nafasi za taasisi zote mwaka ujao na wame tumia wanafunzi wengi tayari mialiko yaku jisajili.

Share